Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia watumishi wa Ofisi yake walioshiriki katika mkutano wa baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo uliofanyika Machi 18, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo Machi 18, 2019 Jijini Dodoma.
 Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu pamoja na waziri anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano wakati wa mkutano huo.
 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi hiyo, anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi wakati wa kikao hicho.
 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi hiyo, anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi wakati wa kikao hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo Bw.Pascal Vyagusa nyaraka za utendaji kazi katika nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na wajumbe wa baraza hilo.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa. akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/2020 wakati wa kikao hicho.
 Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Amina Simbaulanga akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angella Kairuki wakikata utepe nyaraka za utendaji kazi kwa viongozi wa baraza la wafanyakazi wa ofisi hiyo wakati wa mkutano wa baraza lao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki (mwenye koti jeusi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao chao kilichofanyika Machi 18, 2019.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA.MWANDISHI WETU
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, Sera, Bunge na Uwekezaji wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kwa umakini katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na ufanisi wa hali ya juu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi hiyo kilichofanyika Machi 18, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa ufanisi kwani hakuna haki pasipo wajibu, hivyo kila mtumishi azingatie hayo ili kuwa na utendaji wenye manufaa kwa ofisi na Serikali kwa ujumla,”alisema Mhagama
Aidha Waziri Mhagama ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi ikiwemo watumishi wazembe na wenye tabia ya kuchelewa kazini.
“Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,inasisitiza utendaji uliotukuka na bidii kwa kuzingatia adhima ya HAPA KAZI TU, hivyo kila mmoja ajitathimini kwa kina kuona namna anavyoenenda na endapo akaona kuna kasoro arekebishe mapema kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa juu yake,”alisisitiza Waziri Mhagama.
Naye Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki alipongeza watumishi wa ofisi hiyo kwa mafanikio yanayoonekana katika Ofisi hiyo na kutoa wito kwa watumishi kuendeleza jitihada hizo ili kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.
“Kipekee niwapongeze watumishi wa Ofisi hii kwa kuendelea kutekeleza vizuri majukumu ya kila siku kwa weledi kwa kuzingatia ukubwa wa ofisi hii, na tuendelee kutekeleza vya ufanisi ili kuvutia wawekezaji nchini waweze kuona fursa na kuwekeza,”alieleza Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia kikao na kuongezea kuwa Ofisi ya waziri Mkuu inapaswa kuwa mfano katika kusimamia shughuli za mabaraza ikiwa ni sambamaba na kuwataka waajiri kuendelea kuyathamini mabaraza kwa vitendo kwa kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya yenye kuimarisha utendaji wa kazi za kila siku.
“Nawaomba watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira nasi tunatoa shime kwa  waajiri kuendelea kuzingatia umuhimu wa kuundwa kwa mabaraza haya na kuyatumia kwa usahihi kama ilivyokusudiwa” asisitiza Bibi.Tarishi
=MWISHO=
Share To:

Post A Comment: