Na Imma Msumba, karatu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi William Lukuvi amewaagiza maafisa ardhi kote nchini kuanza Rasmi oparesheni maalumu ya ukaguzi wa majengo ili kudhibiti watu wanao kwepa Ulipaji wa kodi ya serikali kwa Maendeleo ya Taifa.

Akizungumza katika Mkutano maalumu wenye lengo la kusikiliza,na kutatua migogoro ya ardhi Wilayani Karatu Mkoani Arusha Lukuvi amesema watu wengi wamekuwa wakiipuuza suala la ulipaji Kodi ya majengo bila sababu za msingi licha ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli kutilia mkazo Katika Ulipaji Kodi kwa maslahi mapana ya wananchi.

Aidha waziri Lukuvi amesema Ni marufuku kwa mtu yoyote mwenye ardhi,shamba lisilo endelezwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka wenye mashamba hayo kuacha kuyakodisha kwa watu masikini ili kujinufaisha wenyewe suala ambalo ni kinyume kwa mujibu wa sheria ya ardhi.

"Ni marufuku kwa watu wasio endeleza maeneo yao kukodisha mashamba kwa maskini ili kujiingizia kipato Kama bado hujajipanga serikali itachukua hati hiyo na kufuta Mara moja kwa ajili ya matumizi mengine"alisema Lukuvi.

Asilimia kubwa ya malalamiko na migogoro ya ardhi Wilayani Karatu imekuwa ikiwakuta wazee na wajane suala ambalo limekuwa changamoto Kutokana na uvamizi na kutofahamu sheria ya masuala ya ardhi nchini.

Msumba news imezungumza na baadhi ya washiriki akiwemo bw:Ezekiel Saitot na Jenipha Richard ambao wamesema ujio wa waziri huyo imekuwa faraja kwa wananchi wengi kwa kupata fursa ya kueleza changamoto zao pamoja na kupata elimu ya baadhi ya vifungu vya sheria kuhusu masuala ya ardhi.

Katika Mkutano huo waziri wa ardhi amesikiliza baadhi ya migogoro ya ardhi Zaidi 300 na kutoa Muongozo kwa wenye kesi mahakamani kuhakikisha wanafatia mashauri yao ili kupata haki zao katika muhimili wa mahakama nchini.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: