Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nigel Msangi akizungumza na watumishi wa Ofisi yake wakati wa zoezi la upandaji wa miti 250 katika eneo la ofisi yao mpya katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma Machi 7, 2019.
 Mtaalam wa masuala ya misitu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Bw.Chambo akionesha moja ya miti aina ya midodoma kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioshiriki katika zoezi la upandaji miti 250 katika ofisi zao mpya zinazoendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.
 Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipanda miti aina ya Midodoma katika eneo la Ofisi zao katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma Machi 7, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Isabela Katondo akitoa karatasi katika moja ya mti wa Mdodoma tayari kwa zoezi la kuupanda aliposhiriki katika upandaji miti eneo la Ofisi hiyo inayoendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nigel Msangi (katikati mwenye shati lenye madoa meupe na meusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya zoezi la kupanda miti katika Ofisi zao mpya Ihumwa Dodoma.

 Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiosha mikono mara baada ya zoezi la kupanda miti katika eneo la Ofisi zao mpya katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nigel Msangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi yake nje ya jengo jipya la ofisi hiyo linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Share To:

Post A Comment: