Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tathimini ya huduma za maji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji nchini
Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tathimini ya huduma za maji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji nchini

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa inatarajiwa kuboresha huduma ya mtandao wa maji taka kutoka asilimia 9.7 % hadi kufikia asilimia 30% ifikapo mwaka 2030
Hayo yamesemwa na Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa Mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa tathimini ya huduma za maji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji nchini
Alisema kuwa kwa kuanzia wameanza kutekeleza mradi wa uboreshaji wa mfumo wa maji taka wenye urefu wa kilometa tatu ambao umeweza kufikia asilimia  40%  na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema kuwa mahitaji ya huduma ya maji taka ni makubwa katika Jiji hilo kwani kwa sasa mtandao huo unapatikana katika maeneo ya kati kati ya Jiji pekee.
“Kutokana na gharama kubwa za uwekezaji kasi ya kuongeza huduma hiyo imekuwa ni ndogo lakini kwa mikakati iliyokuwepo watahakikisha huduma hiyo imeweza kusogeza karibu na wananchi wengi”alisema Mkurungenzi huyo.
Hata hivyo katika kutekeleza sera ya maji Tanga Uwasa imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maji katika wilaya nyingine kama vile Muheza,Pangani,Mkinga na Kilindi.
 “Katika mpango huo hakuna atakayeachwa kwani wananchi wote wanaoishi katika eneo linalohudumiwa na mamlaka hiyo itahakikisha wanapatiwa huduma hiyo”alisema Mhandisi hilly.
Vile vile kwa upande wa udhibiti na uchafuzi wa vyanzo vya maji Tanga Uwasa imeweza kusaidi upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa vijiji vinavyozunguza chanzo cha maji cha Mto Zigi .
“Tumefanikiwa kupeleka  mradi wa maji safi katika vijiji vya Mashawe,Kimbo Shembekeza na vijiji jirani ambavyo vipo karibu na mto zigi ambacho ndio chanzo cha maji”alibainisha .
Share To:

Post A Comment: