Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akiwa ameketi pembeni yake ni Mh. Ridhiwani Kikwete (MB), Mh. Angella Kairuki _ Waziri wa Uwekezaji Mh. Dotto Biteko Waziri wa Madini na Na Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo, wakifuatilia Shughuli ya Kuaaga Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba katika Viwanja vya Gymkhana Bukoba.
 Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
  Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya Bukoba akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
  Mwenyekiti Halmashauri ya  Wilaya Bukoba,Murshidi Ngeze akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
Wakuu wa Mikoa ya Kagera na Dar es salaam Mh. Gaguti na Mh. Makonda wakiweka shada  la maua katika kaburi la Marehemu Ruge kwa Niaba ya Wananchi wa Mikoa yao.


Mwili wa marehemu Rugemalila Gerazi Mutahaba umepumzishwa jana katika Nyumba yake ya Milele , Nyumbani kwao Kable Bukoba Mkoani Kagera, huku mazishi hayo yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Waziri, Wabunge, na Viongozi wa Siasa, Wakuu wa Mikoa wasanii na watu mashuhuri.

Wakiongea mara baada ya shughuli hiyo ya mazishi baadhi ya Viongozi hao wamezidi kumzungumzia Marehemu Ruge kama lulu ya Taifa kwa yale yote aloyafundisha na kuelekeza njia kuwa yafaa kuigwa na kuenziwa kwa namna moja ama nyingine.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akiongea na Michuzi Tv amemuelezea Ruge kuwa, Alikuwa kijana tofauti mwenye maono ya mbali, na ameweza kuyaishi na kutuonyesha kwamba na sisi kama vijana wakati wa ujana tutumie ujana wetu kuhakikisha tunaacha alama hapa Duniani. Pia ameongeza kuwa, kama vijana wa Kitanzania tumeachiwa changamoto kwamba hata kama muda wa kuishi ni mfupi, tukitumia vizuri muda wetu tutaweza kulisaidia Taifa letu la Tanzania.

Nae Naibu Waziri wa Maji Jumaa Awesso amesema Marehemu RUGE kwake ni kama Daktari wa fikra kwani ameweza kubadiri fikra hasi kuwa fikra chanya, na ameweza kuwasaidia Vijana, na akitusisitiza tusiwe vijana Kaa badala yake tusaidiane, kuhakikisha taaluma na Vipaji tulivyonavyo tuinuane katika mambo mbalimbali na kuweza kulisaidia Taifa letu, hivyo katika kumuenzi tunatakiwa kuwa na upendo, ushirikiano na ubunifu kwamba changamoto zipo lakini tunaweza kuzigeuza kuwa fursa, hivyo na sisi kama Vijana tutahakikisha hatuwi Vijana Kaa ili tuweze kusaidiana na kulisaidia Taifa letu.

Katika Upande Mwingine Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya ya Bukoba alipozikwa Ruge amesema Marehemu Ruge amekuwa mhamasishaji mkubwa katika kutumia fursa zilizopo nchini kwa ajili ya kujipatia kipato, kujenga Uchumi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, kupitia fikra alizokuwa nazo na ndoto kubwa za kuinua vijana wenzake, hivyo mchango ake katika Taifa hili utazidi kuwa mkubwa kupitia kuyaenzi matendo yake.

Nae Mh. Murshidi Ngeze Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba anasema Ruge amekuwa mpambanaji ambae ametuachia somo kubwa kwetu, na alama yake haiwezi kufutika ambapo ni kazi yetu kuzingatia yale yote aliyotufundisha na kuyaenzi, hivyo kama Halmashauri wananafikiria kuiomba familia Watengeze Foundation ambayo itayaishi yale yote alokuwa akiyafanya, huku akiongeza kuwa kazi kubwa sasa imebaki kwa Pacha wake Marehemu Ruge, Bwana Joseph Kusaga kuhakikisha anandelea kijenga familia ya Clouds kuwa pamoja na wasione kama Ruge amewatoka kimoyo bali kisura hivyo ni Jukuma la Clouds kama Taasisi kuendelea kuimarika na kusonga mbele.