Thursday, 21 March 2019

Arusha United yajitoa rasmi Ligi Daraja la Kwanza 2018/2019


TIMU ya Soka ya Arusha United (AUSC) maarufu Wanautalii wamejiondoa rasmi kwenye michuano ya Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2018/2019 kwa madai ya kulinda heshima na usalama wa wachezaji, viongozi na mashabiki wao.
Tamko la kujitoa kwa timu hiyo limetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Arusha United, Otte Beda Ndaweka.
“Kumekuwa na hali ya kutokutendewa haki kila timu yetu inapokuwa uwanjani kucheza lakini pia na hata tulipotoa taarifa kwenye vyombo husika lakini hatukuweza kusikilizwa hivyo tumeamua kujiondoa ili kusaidia timuntyin gine kusikilizwa,’’ amesema Ndaweka.
Ndaweka amesema kuna matukio mengi yanaharibu sifa ya Ligi daraja la kwanza.


“Tunaamini kujitoa kwetu kutaleta mchango mkubwa katika usimamizi wa bodi ya ligi daraja la kwanza na hivyo kuchochea maendeleo ya kweli ya soka la Tanzania,” amesema Ndaweka.

No comments:

Post a comment