Friday, 2 November 2018

DC Katambi atinga Stesheni ya Dodoma, Atishia Kuwatumbua


Charles James

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi ametishia kuwatumbua watumishi wa Stesheni ya Treni endapo hawatotekeleza maagizo maagizo yake.

DC Katambi ametoa kauli hiyo leo alipofika katika stesheni hiyo baada ya kupigiwa simu na abiria waliokua wamekwama tangu jana kufuatia treni mbili kukutana.

Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kuzungumza na abiria hao ambao aliwaomba kutulia huku akiuagiza uongozi wa Reli kuwatafutia usafiri mwingine wa kuwapeleka jijini Dar es Salaam pia alikagua mazingira ya stesheni hiyo kutokana na kulalamikiwa na wasafiri hao.

“ Nimepita kukagua mazingira ya stesheni yetu, nimekutana na mambo mengi ya hovyo ambayo yanaweza kutatulika ili kuondoa kero za abiria wetu ambao kimsingi ni Watanzania wenzetu ambao wanalipa kodi ya Nchi yao kwa kulipa nauli.

“ Stesheni kubwa kama hii haina vyoo vya kutosha na vilivyopo vimeziba kutokana na wingi wa vinyesi, maji hakuna pia kwa sababu stesheni inadaiwa na nimewaagiza kulipa deni wanalodaiwa. Na wasipotekeleza basi wajue nitawatumbua,” amesema DC Katambi.

No comments:

Post a Comment