Monday, 22 October 2018

RIDHIWANI KIKWETE AUNGANA NA WASANII KUMZIKA MASHAKA


 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akibadilishana mawazo na msanii maarufu Mzee Chilo kwenye makaburi ya Tabata jana alipozikwa msanii Mashaka.
 Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kwenye maziko ya msanii mwezao Mashaka jana.
Wasanii, viongozi mbalimbali wa kisiasa waliojitokeza kwenye makabuli ya Tabata jana wakati wa maziko ya msanii maafuru wa maigizo Mashaka.


Na Shushu Joel, Dar
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ameungana na wasanii wa kada mbalimbali katika kumzika msanii maarufu wa maigizo nchini Ramadhani Ditopile aliyewai kuwa msanii wa kundi la sanaa la kaole.

Mashaka alifariki juzi asubui wakati akiwa anapata matibabu katika hospital ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Ridhiwani alisema kuwa pengo la msanii huyo ni ngumu kuliziba kwa kipiondi hiki kutokana na jinsi alivyokuwa akifanya kazi zake kwa weredi.

“Mashaka alikuwa si msanii tu kwangu bali alikuwa ni mjomba wa mfano kwani alikuwa akinipatia ushauri mkubwa juu ya kazi zangu za siasa hivyo nimepoteza mtu wa muhimu sana kwangu”Alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa anawapongeza wote waliofika katika kuhakikisha tunamzika ndugu yetu,kwani maziko ni wajibu wetu sote kwani ni ibada.

Aidha mbunge huyo alisema kuwa marehemu mashaka atakumbukwa kwa kupitia kipaji chake cha uigizaji ambapo katika uhai wake aliwai kutamba na kundi la kaole kupitia tamthilia za mambo hayo,kidedea,jumba la dhahabu na nyingine nyingi.

Kwa upande wake msanii maarufu wa uigizaji nchini Mzee chilo alisema kuwa Mashaka alikuwa ni mtu wa pekee katika tasinia ya kuigiza kutokana na kupenda kutumia kipaji chake kuwaelekeza wenzake pindi mnapokuwa katika kazi.

Aliongeza kuwa ni pengo kubwa katika fani yetu lakini kutokana na kuwa hapa duniani tunapita hakuna budi kumuombea kwa Mungu ili apumzike kwa amani.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Abdallah Ditopile,baba yake aliugua ghafla usiku wa kuamkia juzi na kisha kupelekwa hospital ya Amana ambapo alilazwa kabla ya kufariki akiendelea kupatiwa matibabu.

Aidha alisema kuwa baba yake alizidiwa na kupewa rufaa ya kwenda mloganzila lakini wakiwa wanasubili gari ili waelekee huko baba alipoteza maisha”Alisema Abdalaah.

Aliongeza kuwa anawashukuru watnzania wote waliojitokeza kwenye makaburi ya kifamilia yaliyoko Tabata Kinyelezi kwa ajili ya kumzika baba sina la kuwalipa ila Mungu atawalipa kwa wema mliotufanyia wanafamilia.

No comments:

Post a comment