833A8637
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akihutibia wakati wa mahafli ya tisa ya Bodi ya Wataalmu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
IMG_8213
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi , Godfred Mbanyi akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya tisa ya bodi hiyo.
IMG_8220
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi wa Ugavi SR.DKT.Hellen Bandiho akizungumza katika mahafali ya tisa ya bodi yake yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee

833A8650
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban  akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi Bora wa mahafali hayo ambaye amefanya vyema kwenye tafiti yake.
833A8629
 Bahadhi ya Wahitimu wakiwa wamekaa wakisubiri kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
833A8659
 Wahitimu wakiwa wamekaa wakisubiri kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
IMG_8210
 Wahitimu wakila kiapo cha Uadilifu na Maadili mbele ya Mgeni rasmi mara baada ya  kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
IMG_8257
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa bodi hiyo.

Na Humphrey Shao, 

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya Tasisi za Umma kuendelea kufanya Vibaya  katika maeneo ya Ununuzi na Ugavi hili hali bodi ya usimamizi wa masula hayo ipo.
Naibu katibu Mkuu amesema hay oleo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa Mahafali ya tisa ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“ninawaagiza kwa kushirikiana na tasisi zingine zinazosimamia ununuzi wa Umma kama  PPRA,GPSA,PPAA na zingine mlete mpango kazi namna mtakavyofikia tasisi za umma ili kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tuweze kutekeleza jambo hili mapema iwezekanavyo.Lengo ni kuhakikisha tunatumia rasilimali zilizopo ili kuleta Matokeo Makubwa kwa Wananchi” Amesema Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, Godfred Mbanyi  amesema bodi itaendelea na jitihada zake kuhakikisha wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa stahiki ili kuweza kupenya na kuleta ushindani katika soko la ajira la ndani nan je ya nchi .

Mbanyi amesema bodi imeweza kuwatafutia fursa vijana wawili wa CPSP Na Wanafunzi bora wa somo la Procurement and Suply Audit nafasi ya ajira katika tasisi ya Kimataifa ya Nexia SJ Tanzania ambao ni Wataalamu wa Ukaguzi, Hesabu,Kodi, Ushauri wa Kibiashara nk.

Mbanyi alimaliza kwa kutoa rai kwa wahitimu wote watakaotunukiwa shahada ya juu ya fani ya ununuzi na ugavi wafanye hima kujisajili na bodi ili waweze kufanya kazi za ununuzi na ugavi kihalali na kwa mujibu wa sheria .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: