Monday, 1 October 2018

MHE. MABULA AKABIDHI VITABU VYA SH. 12 MILIONI SHULE YA SEKONDARI MKUYUNI

Mhe Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana kwa ushirikiano wa ufadhiri wa taasis ya SOS amekabidhi vitabu 452 vya Sayansi pamoja na masomo yenye michepuo ya Art na uchumi katika shule ya sekondari Mkuyuni vyenye thamani ya shilingi 12,000,000. Vitabu hivyo ni msaada kutoka taasis hiyo ili kuimalisha sekta ya elimu Wilayani Nyamagana. *Nawapongeza wadau wa maendeleo SOS kutoa vitabu 452 shule ya sekondari Mkuyuni msaada unaowezesha utekelezaji wa Sera ya elimu ya Mwanafunzi mmoja Kitabu kimoja* Mhe Mabula amesema

Hafla hiyo imefanyika katika ziara maalum ya Mbunge Jimbo la Nyamagana katika taasis ya SOS akiambatana na viongozi wa SOS wakiongozwa na Kaimu Maneja Ndg. Samson, Mhe . Donator Yusuph Gappi Diwani mwenyeji, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata Mhe. Baluani watendaji wa Serikali Kata na mitaa Mkuyuni pamoja na ujumbe wa Taasis ya First Community Organization.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿


Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: