Wakati anakabidhiwa Ofisi na Kuripoti Kazini kwa Mara ya kwanza kabisa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda alieleza vipaumbele vyake kadhaa, Moja ilikuwa kusimamia Haki na kuhakikisha Mwenye Haki anaipata haki yake kwa inavyostahili.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda anasema Suala la Haki analisimamia kidete kutokana na Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye si tu ameagiza lakini pia Mhe. Rais amekuwa mfano kimatendo katika kusimamia suala la Haki katika utawala wake.

Hatimaye tumelianza Juma la HAKI mkoani Arusha, Katika Tangazo lake la tarehe 03 Mei 2024, Mkuu wa Mkoa ametangaza kuitenga Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ya Wiki hii Mahususi kwaajili ya kusikiliza na Kutatua kero na changamoto za wananchi, Akitoa Rai kwa kila mwananchi mwenye Kuhisi kuonewa, kujitokeza kwa Wingi kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katikati ya Jiji la Arusha.

Baba Mchungaji Godson Abel, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Kati,  anatuma Ujumbe wa Kumtaka Mkuu wa Mkoa Kuwa na Ujasiri katika kuhakikisha watu wanapata haki zao, Akiambatanisha Maneno yake na Maandiko ya Kitabu Kitakatifu cha Biblia cha Yoshua 1.9 akiamini kwamba Mungu mwenye Kupenda Haki na Kutuelekeza kufanya maamuzi katika Haki, atakuwa pamoja na Mhe. Mkuu wa Mkoa Katika siku zake tatu za Kutafuta Haki kwa wananchi walioporwa ama kuminywa kwa haki zao.

Share To:

Post A Comment: