Monday, 8 October 2018

Kauli ya Meya wa Ubungo kuhusu kuhamia CCM

Meya wa Ubungo (CHADEMA), Jacob Boniface.

Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Boniface Jacob amesema kuwa hayuko tayari kuhama wanaozusha waache kuota ndoto zisizo wezekana.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa 'twitter' Jacob ameandika kuwa hayuko tayari kufanya hivyo na yuko tayari kukipigania chama chake hadi kifo chake.

"Waambieni wanaotamani nihamie CCM, nipo tayari kufa nikipigania chama changu CHADEMA na Sipo tayari kuwa takataka kwa kuhamia CCM!, iwe kwa pesa vitisho au kifo acheni kuota ndoto zisizowezekana", amesema Jacob.

Oktoba 6, katika mahojiano yake na  www.eatv.tv Meya Jacob alisema kuwa katika vitu ambavyo hatamani kuvisikia kwa mtu yeyote ni kwamba yeye binafsi ana  mipango ya kuhamia CCM na kusema kauli hiyo ni inalenga kumdhalilisha.

“Unajua wananchi wanapaswa kujua kuwa vyama vya upinzani huwa vinapata tabu sana kwenye uchaguzi hapa nchini lakini niwaambie hatutakata tamaa, tutaendelea kutetea haki zetu", amesema Jacob.

Meya wa Ubungo amekuwa miongoni wa viongozi wa mwanzo kutajwa kuwa wako mbioni kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla ya kushamiri kwa hamahama ya viongozi wa upinzani wanaojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: