Tuesday, 11 September 2018

Madiwani Wengine Wawili wa CHADEMA Arusha Dc Watimkia CCM

Kimbunga cha madiwani na wabunge kuhama hasa vyama vya upinzani na kuhamia CCM kimeendelea kutimka, ambapo jana usiku madiwani wengine wawili wa Katika Halmashauri ya Arusha wamefuata mkondo.

Madiwani hao walioshinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, jioni hii wametangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM hivyo kufanya idadi ya madiwani wa Arusha  Dc waliochukua hatua hiyo kufikia WA tano.

Wakizungumzia sababu za kujiuzulu, Godfrey Mashele wa kata ya Mlangarini na Lembris Mollel wa kata ya Ilboru, wamesea lengo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli.

“Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu udiwani. Nimeandika barua kwa viongozi wa Chadema kueleza uamuzi wangu, kikubwa kilichofanya niamue hivi ni kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli,” alisema Mashele

Mollel pia alitoa sababu sawa na za Mashele na kwamba tayari ameandika barua kwenda Chadema.


Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: