Monday, 6 August 2018

VIONGOZI WACHADEMA TARIME WAWEKA KAMBI ZAIDI YA MASAA MANNE OFISI YA KATA TURWA IILI MAWAKALA WA UCHAGUZI MDOGO WAAPISHWE.


Na Frankius Cleophace Tarime.

Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Tarime pamoja na Wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mkoa wa Mara  Joyce Sokombi na Makamu Mwenyekiti kanda  ya Serengeti CHADEMA ambaye ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Simiyu Gimbi Masaba pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mara Mwl Chacha Heche na Viongozi Wa  chmaa hicho na Mawakala wameweka kambi takribani masaa manne katika ofisi ya kata ya Turwa kwa ajili ya kushinikinikiza mawakala wao waweze kuapishwa kwa mujibu wa kanuni ya  Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Akiongea na Waandishi wa habari katibu wa CHDEMA Mkoa wa Mara Mwl: Chacha Heche amesema kuwa Viongozi ambao ni wasimamizi wa uchaguzi mdogo kata ya Turwa tangu asbuhi wamekuwa wakiwazungusha huku na kule  ili kupoteza muda wao na ili mawakala wao wasiapishwe kwa Mujibu wa Sheria jambo ambalo wamedai hawatakubaliana nalo.

“Kanuni za Uchaguzi zinataka Vyama vya Siasa kupeleka Mawakala kwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi au msaidizi ili kuwaapisha kabla ya siku saba za uchaguzi  lakini sisi tumefanya hivyo tangu asbuhi mpaka sasa hakuna chochote Mkurugenzi wa mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa tumeenda Ofisini kwake hajafanya chochote mpaka sasa lakini kama chama tumeamwandikia barua ili atupe sababu kwa maandishi kwanini hataki kuapisha Mawakala hawa” alisema Chacha.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini CHADEMA Esther Matiko amesema kuwa viongozi wote wameshinda katani hapo badala ya kwenda kufanya shughuli za Maendeleo kwa sababu ya Kiongozi wa Serikali  kushindwa kutimiza wajibu wake hivyo amesema kuwa wataendelea kiukaa maeneo hayo mpaka Majira ya saa Kumi Jioni kama hawajajibiwa kwa Maandhi kwanini Mawakala hawajaapishwa wataripoti Maeneo huska.

“Viongozi Wachache wanaotaka kupindisha Mambo ndo wanaweza kusababisha Vurugu Tarime na sisi kama Viongozi wa Wananchi hatutaki wananchi kuumia sasa waachea waananchi wakachague Viongozi wao” alisema Matiko .

Mpaka habari hii inaenda hewani bado viongozi wa CHADEMA walikuwa bado wameweka kambi katika Ofisi za CHADEMA ili kupatiwa ufumbuzi wa jambo hilo.


Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: