Wednesday, 22 August 2018

Saitoti Zelothe Akutana na Makatibu wa Uvccm Arusha


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana  UVCCM (M) wa Arusha Ndugu Saitoti Zelothe amefanya kikao cha wenyeviti na makatibu wote wa UVCCM katika mkoa wa Arusha.

Agenda kuu katika kikao hicho nikupata taarifa juu ya uhai wa Jumuiya hiyo katika kila wilaya na kuhakikisha kuwa wanakuwa na mahusiano mazuri baina ya viongozi wa jumuiya na chama pamoja na serikali yao wanakuwa na umoja uliotukuka.

Pia ametuma salamu kupitia makatibu na wenyeviti hao kupeleka salam zake za shukran kwa kila kijana katika ushiriki wake wa kufanikisha chama cha mapinduzi kinashinda katika chaguzi zote ndogo zilizo malizika.

Nakuwahasa kushiriki zaidi katika chaguzi ndogo zilizopo mbele yao kwa wakati huu na pia amesisitiza kuhakikisha vijana wanawalinda viongozi pamoja na wanachama wao wakati huu wa chaguzi ndogo

OMARY LUMATO
KATIBU HAMASA UVCCM (M) ARUSHA
21/08/2018

No comments:

Post a comment