Friday, 10 August 2018

PICHA: Rais Magufuli Ashindwa Kujizuia na Kumwaga Machozi Akimuaga Mzee Majuto

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi wakati alipokuwa akiaga mwili wa aliyekuwa msanii nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2018.

Rais Magufuli alifika Karimjee na kujumuika na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na waombolezaji wengine katika kuaga mwili wa nguli huyo aliyefariki dunia jana Jumatano, majira ya saa 2 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili alipokuwa akitibiwa.

Mwili wa Mzee Majuto umesafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga ambako atazikwa kesho Ijumaa, Agosti 10, 2018 mchana.

No comments:

Post a comment