Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amezungumzia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kibeta, mkoani Kagera Siperius Eradius akitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu anayetuhumiwa.

Akizungumza leo Agosti 29 wakati wa Kongamano la Kimataifa la Hisabati linalofanyika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Profesa Ndalichako amedai kusikitishwa na tukio hilo na kwamba Serikali haitamfumbia macho yeyote atakayebainika kuhatarisha usalama wa wanafunzi shuleni, wakiwamo walimu wao.

Amesema mwalimu aliyesababisha mauaji hayo hakutumwa na mtu isipokuwa utashi wake.

Profesa amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vinapofanya kazi yake na kwamba tukio hilo lisitoe tafsiri kuwa shule  siyo mahali salama kwa watoto.
 
 Shule ni sehemu ambayo ni salama kwa hiyo asitokee mtu akafanya vitendo ambavyo hata wazazi wajiulize harugusu mtoto kwenda shule au asiende lakini serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atakayefanya shule ionekane si mahali salama‘-Waziri Ndalichako

Siperius (13) anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na mwalimu akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: