Sunday, 5 August 2018

Jerry Murro, Mghwira wajitokeza kumzika Temba


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mngwira; Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, wameongoza maziko ya aliyekuwa mwandishi wa habari, Hamza Temba,  ambayo yamehudhuriwa na mamia ya waombolezaji nyumbani kwao Masama, Hai, mkoanihumo.

Temba alifariki jana katika ajali ya gari eneo la Magugu mkoani Manyara ambapo alikuwa katika msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ambaye naye alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: