Naibu Katibu Mkuu Dk. AveMaria Semakafu amewataka Maafisa Elimu na Wathibiti ubora kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji na kutoa taarifa kwenye Mamlaka zinazohusika ili changamoto hizo ziweze kupitiwa ufumbuzi.

Dk. Semakafu ametoa kauli hiyo leo Wilaya Magu mkoani Mwanza wakati akishiriki zoezi la ufuatiliaji wa miradi inayofadhiliwa na washirika wa Maendeleo kuhusu  ufundishaji na ujifunzaji AJESR.

Dk. Semakafu amesema suala la ufuatiliaji kwa viongozi waliopewa Mamlaka ni la lazima kwani itasaidia zaidi kubaini changamoto lakini pia ni sehemu ya uwahibikaji katika kutumiza malengo ya Taifa.

“ Viongozi  ni lazima tuwajibike katika kushughulikia masuala ya wananchi na siyo kusibiri kiongozi wa juu aje atoe maelekezo ndiyo tuanze kukimbizana, mfano wewe mthibiti ubora wa shule, au Afisa Elimu unakagua shule zako? unatatua changamoto au unasubiri mpaka Mkurugenzi wa Halmashauri atoe maelekezo?” Alisisitiza Dk. Semakafu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba ameahidi kuendelea kufanyia Kazi changamoto mbalimbali zilizopo katika Halmashauri hiyo ili Taifa liweze kusonga mbele.

Mwalibwa amesema hakuna jambo ambalo litaweza kuwa mbadala wa Elimu, Elimu ni kila kitu sasa ikivurugwa Elimu Taifa haliwezi kusonga mbele.

“ Tukiwa na misingi mizuri ya Elimu lazima Taifa tutafanikiwa, changamoto zipo na ndiyo maana viongozi tupo kama changamoto zisingekuwepo basi hata viongozi tusingrkuwepo,”alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
16/8/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: