Saturday, 14 July 2018

Wanigeria 400 wakwama Russia baada ya kuuziwa tiketi feki

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Russian liitwalo “Alternative” limefichua kwamba Wanigeria wapatao 400 waliokwenda kushuhudia Kombe la Dunia nchini Russia, wamekwama nchini baada ya kugundulika kwamba waliuziwa tiketi feki.

Kati ya hao, 60  wamelazimika kulala nje ya ubalozi wa Nigeria nchini humo ambapo ubalozi huo umesema utawahifadhi hapo kwa siku mbili tu na haujasema nini kitafanyika baada ya muda huo kwisha.

No comments:

Post a Comment