Saturday, 21 July 2018

PICHA: Kangi Lugola na IGP Simon Sirro wakutana uso kwa uso

Waziri wa  Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola jana amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Sirro na Maofisa wengine Wakuu wa Jeshi hilo, Makao makuu ya Polisi Dar es salaam.

Waziri Lugola amekutana na IGP Sirro kukiwa na mfululizo wa maagizo aliyoyatoa ikiwemo kumtaka IGP Sirro amwambie kama wamewashindwa majambazi kutokana na kulazimika shughuli nyingi kufungwa inapofika jioni kwa kuhofia kuvamiwa.

Jambo la pili ilikuwa ni kutaka maelezo ya alipo Mbwa maalum wa Kikosi cha Bandari ambapo mpaka  jana asubuhi ya  July 20 2018 alikuwa hajapatikana. 

Baada ya Kikao hicho, Lugola alisema kilikuwa ni cha majumuisho ya zaiara zake ambapo ametoa mwezi mmoja zaidi kwa jeshi la polisi ili waandae ripoti kuhusiana na changamoto ya mbwa wa Bandarini pamoja na mpango mkakati wa kuwawezesha wananchi kufanya kazi zao usiku walau kwa baadhi ya maeneo.

No comments:

Post a comment