Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson amewataka wazazi wenye watoto wa kike wenye Ulemavu kuwapeleka Shule ili wapate haki yao ya kupata Elimu wakati Serikali inaendelea kutatua Changamoto za Miundombinu zinazowakabili Mashuleni.

Dk Tulia amesema hayo katika Kongamano la kujadili maswala yanayowahusu Walemavu jijini Dodoma lililoandaliwa na mfuko wa misaada wa IKUPA Trust Fund huku akisisiiza Jamanii kuwaona watu wenye ulemavu kama watu wengine na kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga katika shughuli mbalimbali.


Kongamano hilo litafanyika kwa Siku mbili huku likiwashirikisha Wadau pamoja na walengwa Watu wenye Ulemavu kutoka mikoa mbalimbaali ili kuweza kujionea changamoto zinazowakabili katika jamii zetu

Aidhaa Dk.Tulia ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais Dkt.Magufuli inavyoendelea kuthamini Watu wenye Ulemavu ambapo aliamua kumchangua Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa ambaye ndio muanzilishwa wa IKUPA Trust Fund.


Pia amesema kuwa kukosekana kwa Wakalimani wa vitendo kwa Watu wenye Ulemavu imekuwa moja ya changamoto kubwa nchini ambayo inapelekea kuwapa ugumu wahudumu kwa kuweza kuwasaidia katika jambo lolote lile.

Hata hivyo amesema kuwa ni Jukumu la viongozi na wadau mbalimbali kusimama na kuwaelimisha wananchi na kukemea vitendo ambavyo vinatokea kwa Watu wenye Ulemavu maana kumekuwa na hisia tofauti tofauti mtu anapotokea Mtu anataka kumuoa Binti mwenye Ulemavu jamii inaanza kushangaa na kutoa maneno ya Kejeli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: