Monday, 23 July 2018

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Atembelea Makao makuu Tume ya Nguvu za Atomiki

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ametembela Makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomu yaliyopo Mkoani Arusha siku ya Ijumaa tarehe 20 Julai 2018. Katika ziara yake, Naibu Katibu Mkuu   amezungumza na uongozi wa Tume juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji wa Tume. Pia alipata fursa ya kuelezwa na kuona mipango mbalimbali mahususi ya kimaendeleo ya Tume.

Baada ya mazungumzo hayo alipata muda wa kutembelea na kukagua  maabara kubwa na Kisasa ya Tume  ya Nguvu za Atomu iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya tano kwa kugharibu jumla ya kiasi cha Shs Bilioni 2.36 sambamba na Bilioni 11  za vifaa Pamoja na Mafunzo kwa watafiti zilizofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Maabara hii itakamilika rasmi mwezi September, 2018 itasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye usimamizi na udhibiti wa mionzi  hapa nchini na na nchi zingine za Afrika Mashariki na Kati. 

Naibu Katibu Mkuu aliambatana na baadhi ya Wafanyakazi wa Tume hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tume  Prof. Lazaro S.P. Busagala katika kutembelea na kukagua ujenzi wa maabara hiyo
 Mkurugenzi wa Tume ya nguvu za Atomiki Prof.Lazaro S.P Busagala akimpatia maelekezo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe.
 Mtaalamu katika  Makao makuu ya Nguvu za Atomiki Bi. Sara Lema Akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akipokea maelekezo toka kwa Mtafiti wa Tume  hiyo Bi. Furaha Chuma.


 Muonekano wa maabara hiyo kwa ujenzi ulipofikia kwa upande wa nje.

No comments:

Post a comment