Tuesday, 3 July 2018

Mwigulu amlilia Prof. Majimarefu


MBUNGE wa Iramba Magharibi (CCM) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani alieaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

Kupitia Twitter, Mwigulu ameandika;

“Maandiko matakatifu yanasema, mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, tumempoteza kaka, ndugu na rafiki Comrade Stephen Hilary Ngonyani (Prof. Majimarefu), tumempoteza kiongozi na kada kweli kweli wa Chama Cha Mapinduzi. Mungu akupumzishe kwa Amani.”

No comments:

Post a Comment