Na Mwandishi Wetu
01/07/2018


MTENDAJI MKUU WAKALA WA MAJENGO TANZANIA(TBA) Arch;  ELIUS ASANGALWISYE MWAKALINGA AONYESHA UWEZO MKUBWA KATIKA KUSIMAMIA  UBORA WA MIRADI  NA KUOKOA FEDHA ZA UMMA.



Nimepitia taarifa ya maendeleo ya Mradi mkubwa wa nyumba za Makazi Ujulikanao kama MRADI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA,
Kilichonifurahisha ni namna ambavyo Mtendaji mkuu wa  Arch. Mwakalinga alivyochukua hatua mbalimbali katika kuokoa fedha za Umma  na kuhakikisha Mradi unatekelezwa kwa Ubora [pamoja na changamoto mbalimba wanazokutana nazo wakati wa Utekelezaji wa Mradi,

Katika Taarifa hiyo fupi ya Utekelezaji wa Mradi huo unaotekelezwa kwa pamoja na Wizara ya Ujenzi  Uchukuzi, na Mawasiliano, Wizara ya fedha  na Wakala wa majengo Tanzania  TBA Kila mmoja akiwa na majukumu yake maalumu  kwenye Mradi huo.
.
Utekelezaji wa Mradi huo ulianza kwa wataalamu wa TBA kufanya Ubunifu wa  majengo na wale wa  BICO-UDSM  Kufanya  uchunguzi wa  udongo ili kubaini uwezo(bearing capacity) wa kuhimili uzito wa majengo  unaotarajiwa kujengwa, wakati huo huo wakala wa majengo aliendelea kufuatilia  vibali kutoka mamlaka mbalimbali  zikiwemo NEMC, Manispaa, AQRB na ERB Haya yote yalifanyika ili kukidhi mahitaji ya kisheria kwenye sekta ya ujenzi.

Mradi huu una jumla ya vitalu  vitano (5Blocks) vitalu vinne  vina ghorofa  nane na mija ina ghorofa tisa na pia kitaru kimoja kinabeba  kaya 126 ni mradi mkubwa na wakisasa kwa hapa kwetu nchini. Mradi mzima unauwezo wa kubeba Kaya 656 maana vitalu vinne vinabeba kaya 512 kitalu kimoja kinauwezo wa kubeba kaya 144,.

Hadi sasa mradi umeweza kukamilisha ujenzi wa msingi kwa Asilimia mia moja ( 100%) na Asilimia 35% kwa kazi ya juu ya msingi, Kama kawaida yake Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo Tanzania  Arch , Mwakalinga amekuwa akifanya majaribio ya uchunguzi wa  wa zana mbalimbali kwenye maabara  mbalimbali kati kuhakikisha  vifaa vya ujenzi kwenye mradi huo ni zenye Ubora unaohitajika kwa mujibu wa maelekezo ya Kitaalamu, Vifaa vinavyochunguzwa mara kwa mara ni kama vile Mchanga, Kokoto, nondo  na zege na maabara zilizotumika ni kama vile  Chuo kikuu cha Dar es Salaam, BICO, na DIT,

Tathimini ya gharama za mradi  zilizotumika mpaka sasa  kulingana na tathimini iliyofanywa na wakadiriaji majengo  Mradi umeweza kugharimu  kiasa Cha 14,497.144,106,.65 (Shilingi za kitanzania) na Makisio ya gharama za kumaliza mradi (FRAME) Mradi una jumla ya  bock tano  zenye jumla ya floor arobaini  na moja  mpaka sasa  kati ya  hizo  flppr kumi  na  mbili  zimekamilika  kwa hatua  ya  frame, Makisio kwa floor  moja ni shilingi  438,611,875,00 hivyo  basi  makisio  ya  gharama ili kuweza kumaliza  floor zilizobaki (floor 29) ni 12,719,744,375.00( Shilingi bilioni  kumi na mbili  milioni mia saba kumi na  tisa laki saba arobaini na nne mia tatu sabini na tano)

HAPA NDIPO NINAPO MPONGEZA  ARCH. ELIUS ASANGALWISYE MWAKALINGA

.
Mtambo wa Kisasa wa Kuzalisha Zege umeweza kudhalisha  kiasi cha mita  za ujazo 5799.800 kwa miradi mbalimbali ya mkoa wa DSM  kama vile  magomeni kota, Ukonga, TPA, Bandari, Osha na Ujenzi wa  nyumba ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete unaofanyika Kawe
Maamuzi ya kununua Mtambo wa kuzalisha zege yaliyofanywa na wakala wa majengo Tanzania umeleta faida nyingi sana na kuokoa fedha nyingi pia moja ya faida hizo ni (a) Kupungua kwa gharama za uzalishaji  wa zege
(b) Kuokoa muda wa utendaji kazi
(c)Ubora wa zege kwa kuwa TBA wanazalisha wenyewe
(d) Matumizi sahihi ya malighafi kama kokoto, mchanga,na simenti.

CHANGAMOTO NA UTATUZI WAKE.
.
Arch E. A Mwakalinga akiwaongoza wataalamu wenzake katika mradi huu alikumbana na changamoto mbalimbali  ikiwemo kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi  mfano,  bei ya awali ya nondo  ilikuwa  shilingi milioni moja  laki sita  na ishilini  mapa milioni moja na laki nane  na bei ya  sasa  ni shilingi  milioni mbili laki mbili na  nusu kwa tani,
Lakini kwa weledi mkubwa Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo Arch. Mwakalinga aliweza kutatua changamoto hii kwa kupata wazabuni ambao wana supply vifaa kwa  bei  nafuu na  maamuzi yenye busara kwa kununua mtambo  na magari  ambayo yatapunguza  kupata kwa  gharama za Mradi.



KUOKOA FEDHA ZA UMMA.
.

Kwa kutumia wakala wa majengo Tanzania chini wa uongozo wa kizalendo wa Arch . Mwakalinga Serikali imeweza kuokoa mabilioni ya fedha  Mfano wa miradi hiyo ni kama ifuatayo,


Miradi waiyookoa fedha za umma ni
.

1. Ujezi wa Hostels chuo kikuu - Wakala wa majengo Tanzania TBA mejenga kwa 10b against zaidi ya 80b za Wakandarasi wapigaji

2.Ujenzi wa ihungo Sec wakala wa majengo Tanzania TBA walijenga kwa  13b against 40b za wapigaji

3.Ujenzi wa Hospital Geita Wakala wa majengo Tanzania waliweza kujenga na kukamilisha kwa   17b against 75b ya private contractors (Wapigaji)

4. Ujenzi wa Hospital Chato Wakala wa majengo Tanzania walijenga kwa 15b against 65b private( Wapigaji)

5. Ujenzi wa Hospital Simiyu  Wakala wa majengo Tanzania waliweza kujenga na kukamilisha kwa  12b against 36b private(Wapigaji)

Ukipiga hesabu utaona wameokoa kiasi kikubwa cha fedha ya serikali ambayo imeingia kuwahudumia wananchi kwenye miradi ya maendeleo.Kwanini mimi David Maphone nisipoteze muda wangu kumpongeza Mzalendo wa aina hii ya Arch Mwakalinga
Jambo kama hili haliwezei kuwafurahisha wezi waliokuwa wakitaka Wakala wa Majengo Tanzania TBA aendelee kukodi mitambo na magari ili kuongeza gharama za Mradi na wapo hata waheshimiwa wabunge wanatumika kufanya hujuma hizi, Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo amemuunga mkono Rais Magufuli kwa kununua Mtambo sio kukodi kwa sababu hata Mhe Rais alipinga wazo la wabunge kukodi Ndege na badala yake aliamua kununua kabisa ili kukwepa gharama na kutuleteaa maendeleo ya uhakika.

.
Katika kuunga mkono TBA maendeleo ya mradi wa Magomeni kota na Taarifa ya TBA  Mbunifu Majengo anayeheshimika sana kwa uwezo wa kiutendaji kupitia mchangu wake kwenye moja ya Group za WhatsApp
Arch. Humphrey Zachary Killo amesema ''Mradi huu ni muhimu kwa wakazi wa DSM na maendeleo yake ni makubwa tuwaunge mkono'


KWA UDANI ZAIDI USIKOSE KUSOMA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MRADI ITAFUATA
Share To:

msumbanews

Post A Comment: