Tuesday, 3 July 2018

Mbunge Profesa Majimarefu Kuagwa Kesho July 4

Aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu, ataagwa kesho na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea jimboni kwake Korogwe kwaajili ya maziko.

Kaka wa marehemu, Hilary Ngonyani amesema kuwa taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitatangazwa baadae, ikiwemo mahali itapaofanyika ibaada ya kuaga mwili wa marehemu Maji Marefu, pindi watakapokamilisha mawasiliano na ofisi ya Bunge.

“Mwili utabaki Muhimbili leo, hadi hapo kesho tutakapoaga katika viwanja ambavyo taarifa itatolewa badae baadaya ya kukamilisha mawasiliano na Ofisi ya Bunge, ambapo ataagwa na wakazi wa Jijini Dar es salaam pamoja na wabunge wenzake na baadaye tutaanza safari ya kuelekea Korogwe kwaajili ya shughuli ya Mazishi”, amesema Hilary Ngonyani.

Taarifa za kifo cha mbunge huyo ziliripotiwa usiku wa Julai 2, majira ya saa 3:20 na Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.

June 6, 2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu hospitali ya taifa pia.

No comments:

Post a Comment