Monday, 9 July 2018

Kauli ya Mwigulu Nchemba Baada ya Ndege Mpya ya Dreamliner Kutua Nchini

Rais Dr. John Pombe Magufuli jana  ameipokea ndege mpya aina Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini DSM.

Baada ya mapokezi hayo baadhi ya watu wamekua wakitoa pongezi zao akiwemo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya NdaniMwigulu Nchemba ambapo ameandika katika ukurasa wake Twitter  kuwa; 

“Historia nyingine imeandikwa, tunakila sababu ya kujivunia maendeleo haya, Asante serikali yetu chini ya Rais J.Magufuli kwa hatua hii nyingine kubwa ya kuipeleka nchi yetu mbele katika usafiri wa anga.”

No comments:

Post a Comment