Vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo vimeanza mazungumzo ya kushirikiana  katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, 2018 ikiwa ni  Mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo  wa ubunge jimbo la Buyungu na Kata 79

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam, huku ACT ikiwakilishwa na Omar Said Shaaban ambaye pia ni rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS).

Timu ya Chadema katika mazungumzo hayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Oganaizesheni  na Uchaguzi,

 Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema baada ya kumalizika kwa mazungumzo wamewaachia jukumu Chadema kwenda kujadiliana.

“Tulichokizungumza wenzetu wa Chadema  wanayajadili katika ngazi ya sekretarieti kabla ya kufanya makubaliano ya mwisho. Hekima inatutaka kuwasubiri wenzetu wajadiliane, waafikiane na kisha tufanye makubaliano ya mwisho. Tunasubiri,” amesema Shaibu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: