Friday, 1 June 2018

Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi

Waziri wa Elimu Nchini Afrika Kusini, Angie Motshekga amesikitishwa na kwaya ya kundi moja la wanafunzi ambao wamekuwa wakiimba wakiwa watupu.

Amesema kuwa amesikitishwa sana baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana kama “inkciyo”.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na maadili ya tamaduni za taifa hilo hasa kwa watoto wa kike.

“Tabia hiyo mbaya sana inaenda kinyume na maadili ya tamaduni zetu, mtoto wa kike anafaa kuthaminiwa na si kufundishwa mila potofu,”amesema Waziri Motshekga

Hata hivyo, mkufunzi wa Kwaya hiyo ya wanafunzi amesema kuwa ni fahari kubwa kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa huku wasichana wakiwa watupu.

No comments:

Post a comment