Saturday, 9 June 2018

Wasira - Zitto Kabwe ipumzishe CCM


Aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira amemtaka Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuipumzisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukurasa wake wa ‘twitter’ kuhusiana na mjadala wa Maaskofu wa KKKT.

Wasira akizungumza na eatv.tv amefunguka kuwa Chama cha Mapinduzi ni wanachama na vikao na hakuna kikao chochote kilichokaa kujadili waraka huo wa maaskofu na kumtaka Zitto asiwatuhumu kwenye mitandao ya kijamii.

“Zitto anaihusisha CCM kwenye vitu ambavyo hatujajadili tukiwa kama chama kwani tuna vikao vyetu halali na huwa taarifa inatolewa lakini kwa hilo anakosea”, amesema Wasira.

Mwanzoni mwa wiki hii ilisambaa barua mitandaoni ikiwataka viongozi wa Kanisa la KKKT kuwataka kuufuta waraka uliotolewa Pasaka ndani ya siku kumi, ambao suala ambalo liliibua mijadala katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa watu hao alikuwa ni Zitto Kabwe na Humphrey Polepole na jana Juni 8, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba katika mkutano wake na waandishi wa habari alikanusha barua hiyo.

No comments:

Post a Comment