Friday, 8 June 2018

Serikali: “Tutapandisha mishahara hali ikiruhusu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa serikali itaweza kuboresha maslahi ya watumishi wa umma nchini kwa kuongeza mishahara kulingana na uwezo wa Serikali.

Waziri Mkuchika, amesema hayo leo Juni 8, 2018 Bungeni, Jijini Dodoma akielezea ni kwa namna gani Serikali inawajali watumishi swali lililoulizwa Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige na kuongeza kuwa Serikali inafanya jitihada za kuwajali watumishi kwa kuwapa mikopo, mafunzo na kudhamini masomo kwa baadhi ya watumishi wanaosoma taaaluma mbalimbali.

“Kujali mtumishi sio lazima fedha, hata ukimpeleka kwa mafunzo umemjali mtumishi, niseme tu kifupi kwamba tunaendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma lakini kwa upande wa mishahara, tutaipandisha hali ya nchi ikiruhusu”, amesema Mkuchika.

Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali haitasubiri sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) ili itangaze kupanda kwa mishahara bali muda wowote amabapo itajiridhisha na hali ya mfuko wa serikali basi itapandisha mishahara.

No comments:

Post a Comment