Friday, 1 June 2018

NAIBU WAZIRI APONGEZA UJENZI NA UBORESHA WA KITUO CHA AFYA USA-RIVER


Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kusimamia vyema ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa- River  uliolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika umbali mdogo na kupunguza msongamano kwenye Hospitali ya Wilaya Meru iliyopo Tengeru na Hospitali ya Rufaa Mount Meru.

Mhe.Naibu waziri Ndugulile amesema hayo alipokuwa kwenye ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati alipo fanya ziara kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Meru ya hali upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya Afya na zahanati na kufurahishwa na utekelezaji uliofanyika .

Aidha Mhe.Ndugulile  amesema Serikali ya awamu ya tano imeipa kipaumbele Afya ya mwananchi kwa kuhakikisha anapata huduma bora za afya kwenye umbali unaofikika hivyo baada ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya Nchini Serikali inatatua changamoto ya uhaba wa watumishi  wa Afya kwani mpaka sasa imetoa kibali cha kuajiri watumishi wa afya wapatao 8000 kati yao 6,200 wataajiriwa kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha milioni 500 iliyotumika kuboresha kituo hicho cha Afya Usa - River kwa kufanyika ujenzi wa majengo  mapya ambayo ni jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti, kichomea taka  pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo ambayo ni Jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje  (OPD), jengo la duka ambalo awali lilitumika kama kama jengo Maabara,Jengo lenye  pande mbili likitumika kama wodi ya wanawake na wanaume  .                                                                                                                                                                                                                                           
PICHA ZA TUKIO.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine pamoja na viongozi wengine akikagua ujenzi na uboreshaji wa kituo cha Afya Usa- River.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Timoth Wonanjina Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara wakitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa kwenye Kituo cha Afya Usa - River.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akimuhoji mama mgonjwa juu ya huduma ya dawa kwenye kituo cha Afya Usa- River.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Katibu Tawala kwenye Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava juu ya utekelezaji wa maagizo ya ziara yake ya awali.
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akipongeza namna ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa- River  ulivyosimamiwa vyema .
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akimuhakikishia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetekeleza Ujenzi huo na ukarabati wa Kituo cha Afya Usa- River kama Serikali ilivyokusudia. 
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akimpa mkono wa pongezi  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri usimamizi mzuri Ujenzi huo na ukarabati wa Kituo cha Afya Usa- Rive kama Serikali ilivyokusudia. 

No comments:

Post a comment