Wednesday, 6 June 2018

Mkoa Wa Mbeya Umeagizwa Kutenga Mapato A Ndani Kwaajili Kuratibu Shughuli Zinazo Halmashauri Na Wilaya.

Halmashauri za wilaya mkoani Mbeya zimeagizwa kutenga bajeti kutoka vyanzo vya mapato vya ndani kwaajili ya Kuratibu shughuli za vyama vya ushirika na kuufanya ushirika kuwa agenda ya kudumu.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Amos Makalla ametoka agizo hilo kwenye Hotuba yake iliyosomwa na Kaimu katibu tawala wa mkoa,Costantine Mushi kwenye hafla ya kufunga Jukwaa la Vyama vya ushirika mwaka huu lililofanyika kwa siku mbili. 
 
Halmashauri zimetakiwa  kuhakikisha Elimu ya ushirika inatolewa kwa vyama vyote ili kuwezesha Ushirika kuwa endelevu sambamba na wananchi kutambua umuhimu
 
Pia kutoa agizo kwa kila Afisa ushirika kutekeleza majukumu kwa wakati hususani kwa kuwa karibu zaidi na vyama vya ushirika huku pia kwa watendaji wa vyama hivyo wakitakiwa kuwa waadirifu na wasioungana na viongozi wanaopenda kujinufaisha wao badala ya wanachama.

Kwa upande wa Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Mbeya,Bibi Angel Maganga amevitaka vyama vya ushirika kuandaa agenda za Kodi kwenye mikutano

No comments:

Post a comment