Serikali imesema mfumuko wa bei umeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 3.8 Aprili mwaka huu, kutoka 5.3 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na mtumizi kwa mwaka 2018/19.

“Mheshimiwa Spika kupungua kwa mfumuko wa bei kulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula, utulivu wa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu ya kigeni, kuimarisha kwa uzalishaji wa umeme,” amesema Dk. Mpango.

Pia amesema serikali inapitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali (CAG) na kwamba itazingatia ushauri alioutoa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: