Ghana imevunjilia mbali chama cha soka baada ya rais wake kunaswa katika video akionekana akipokea 'zawadi ya pesa'.

Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka Ghana, Mpaka sasa hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.

Waziri wa michezo Isaac Asiama amesema chama hicho 'kimevunjiliwa mbali mara moja' mtandao wa GhanaWeb umeripoti.

Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika.

Katika makala hiyo ndefu, iliopewa jina 'wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida', ilikabidhiwa kwa maafisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

Mustapha Abdul-Hamid, waziri wa habari Ghana amesema serikali "imeamua kuchukua hatua za mara moja kukivunja chama cha soka Ghana GFA", akitaja "kuenea kwa muozo unoaonekana".

Amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, kukisubiriwa kuundwa chama kipya.

Katika taarifa yake GFA kimesema itatoa ushirikiano katika uchunguzi wowote, Nyantakyi ni makamu wa rais wa shirikisho la kandanda Afrika na pia mwanachama katika baraza la Fifa - taasisi inayosimamia soka duniani.

Tangu achukuwe uongozi wa chama cha GFA, ametuma ujumbe mkuu dhidi ya kupambana na rushwa.

Hatahivyo katika makala hiyo ya upekuzi inamuonyesha akiweka pesa hizo $65,000 "za kununua vitu" katika mfuko mweusi wa plastiki.

Kitengo cha upekuzi cha BBC, Africa Eye, kimeipata kanda hiyo ya video, Kikosi cha mzalishaji filamu hiyo walimuita Nyantakyi katika hoteli ya kifahari huko mashariki ya kati kwa ahadi kuwa atakutana na mfanyabiashara tajiri aliye na hamu kuingia katika mkataba wa uwekezaji na GFA.

Mr Nyantakyi alijadiliana na kuandika mkataba huo wa ufadhili kwa niaba ya chama cha soka Ghana ambao ungeruhusu sehemu ya ufadhili huo kuelekezwa katika kampuni anayoimiliki.

Waandishi wanasema iwapo makubaliano hayo ya uongo yangefanikiwa, huenda angenufaika kwa dola milionni nne na nusu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: