Friday, 8 June 2018

Dk Shika amtambulisha rasmi Msanii wake

Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amefunguka na kutangaza nia ya kujihusisha na masuala ya muziki nchini Tanzania hasa upande wa kuwasimamia wasanii wachanga na wakubwa.

Dkt. Shika ametoa kauli hiyo leo Juni 08, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema siku si nyingi atatangaza jina rasmi ya label yake ambayo itakuwa inajuhusisha na kusimamia kazi za wasanii wa BongoFleva huku akidai lengo lake kubwa ni kutaka kutimiza ndoto za kila mmoja kupitia sanaa.

"Sasa tutaelewana tu na kabla hatujaanza na masuala ya viwanda 30 nilivyo vitaja na 'different services', kwa sasa ninaanza na 'music industry' na tunaanzia kwa msanii mmoja ambaye anaitwa Godson anayetokea Songea na hili nina uhakika watanzania watafurahi na kufuta 'stress' mbalimbali zilizokuwa zinawasumbua", amesema Dkt. Shika.

Pamoja na hayo, Dkt. Shika ameendelea kwa kusema "nipo tayari kuwasimamia wasanii wengine watakaopenda lakini ninaanza na huyu mmoja na nina uhakika atawafunika wasanii wengi, kwa hiyo jaribuni kumfuatilia".

Kwa upande mwingine, Dkt. Louis Shika amesema ukimya wake wa kipindi kirefu umetokana na yeye kuhangaikia kuingiza fedha nchini kutokea nje ili aweze kutimiza azma yake aliyokuwa ameitangaza hapo awali.

No comments:

Post a Comment