Posted On: May 24th, 2018
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Christopher J. Kazeri alipotembelea ubomoaji na uondoaji wa vizuizi vya barabara maeneo ya Leganga Usa-Rivar iliyofungwa na baadhi ya wananchi wanaomiliki maeneo karibu na barabara hiyo kwa kujenga majengo amewaasa wananchi wa Halmashauri hiyo kufuata taratibu za uendelezaji wa maeneo  ili kuepuka adha zitakazojitokeza ikiwemo adhabu za kisheria .
Mmoja wa wahanga wa ufunguzi huo wa barabara unaoendelea kwa kubomoa majengo ( jina limehifadhiwa) amesema yeye amechukulia ufunguzi wa barabara hiyo kama maendeleo ya Mji.
Naye Judas T. Mahuma ambaye ni Afisa Ardhi Mteule kwenye Halmashauri hiyo amefafanua kuwa kama kuna maendelezo yoyote yanayotakiwa kufanyika kwenye ardhi ya jumla lazima mhusika mwenye eneo kwenye ardhi hiyo ya jumla apate kibali cha kufanya muendelezo huo kutoka kwenye Halmashauri, hii ni kwa mujibu wa kanuni za ujenzi  mijini za mwaka 1991 .
Aidha Mahuma amesema faida za kufuata utaratibu wa uendelezaji  wa ardhi ni pamoja na uwepo wa makazi yaliyopangiliwa yatakayo rahisisha utoaji wa huduma za kijamii akitoa mfano wa huduma za barabara zinazo muezesha kila mtu kupita bila kikwazo pamoja na huduma nyingine kama shule na Hospitali kuwa kwenye mpangilio maalumu ambao hautokuwa na usumbufu kwa wakazi wengine,pia kuimarika kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao mfano pale linapotokea janga la moto uokoaji wa watu na mali utakuwa rahisi kwa maeneo yaliyopangiliwa.
Mhandisi wa majengo kwenye Halmashauri hiyo amesema taratibu za kupata kibali cha ujenzi mwananchi anatakiwa kufika ofisi ya ujenzi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru akiwa na nyaraka za umiliki/mhutasari wa kijiji unaohusu umiliki wa eneo pamoja na ramani ya ujenzi anaotarajia kuufanya ambapo atajaza fomu ya maombi ya kibali cha ujenzi na kusubiri taratibu za ukaguzi kukamilika ili apewe kibali.
PICHA ZA TUKIO.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: