Friday, 11 May 2018

Wadaiwa Sugu Wa Nssf K’njaro Kupandishwa Kizimbani

Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro
Waajiri 100 wa sekta mbali mbali mkoani Kilimanjaro watafikishwa Mahakamani kama watashindwa kulipa deni la michango ya Wafanyakazi wao la zaidi ya shs.1.6bil/= baada ya kushindwa kuwasilisha michango hiyo wanayodaiwa na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.

Meneja wa NSSF mkoani Kilimanjaro Bw Jamal Mchula amesema wiki ijayo wataanzisha kampeni ya wiki mbili ya kuwadai waajiri hao na baada ya muda huo sheria itachukua mkondo wake bila kujali uwezo wa mwaajiri.

Bwana  Mchula amesema hayo wakati wa mafunzo ya waajiri 200 kati ya 2,000 mkoani kilimanjaro juu ya mabadiliko ya sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imewekwa saini hivi karibuni na rais john pombe magufuli.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi Agness Hokororo ameitaka nssf kuacha kuanya kazi kwa mazoea kwa kutowachukulia hatua wadaiwa sugu na waajiri watekeleze wajibu wao wa kuwasilisha michango hiyo ili kuondoa malalamiko ya wafanyakazi.

No comments:

Post a comment