Thursday, 10 May 2018

Ujumbe wa Professor Jay baada ya Sugu kutoka gerezani

Mbunge wa Jimbo la Mikumi na rapper mkongwe, Joseph Haule aka Professor Jay ameungana na watu wengine mbalimbali wakiwemo viongozi wa Chadema katika kufurahia kutoka kwa Sugu gerezani.
Professor ametumia mtandao wa Instagram katika kuonyesha hisia zake hizo huku akimkaribisha Mbunge mwezake huyo wa Jimbo la Mbeya Mjini.
Kupitia mtandao huo Jay ameandika, “MUNGU ni wetu sote… Hatimaye Yametimia💪💪Karibuni sana URAIANI Makamanda Wetu SUGU na MASONGA✌✌.”
February 26 ya mwaka huu Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano gerezani akiwa na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga kwa kosa la kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

No comments:

Post a Comment