Tuesday, 22 May 2018

Spika Ndugai amkaribisha tena Sugu bungeni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo, Mei 22 amemkaribisha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) Bungeni jijini Dodoma.

“Mh. Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi, Karibu tena Bungeni na Karibu uuliza swali lako,” amesema Spika Ndugai.
February 26, 2018, Sugu alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya.
Sugu aliachiwa huru kutoka gereza la Ruanda, Mbeya Mei 10 alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano.

No comments:

Post a comment