Kwenye mkutano mkuu wa dharura wa Simba unaoendelea mchana huu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Serikali imebariki mabadiliko ya katiba yanayofanyika kwenye mkutano huo ili kubadili mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo.

Serikari imetoa baraka hizo kupitia kwa Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akitoa neno juu ya mabadiliko hayo ambapo amesema Simba imefuata taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali hivyo kila kitu kinfanyika kwa mujibu wa sheria.

''Mabadiliko yanayofanywa na klabu hiii ni mazuri na yataleta maendeleo kwenye soka la Tanzania, hivyo hayana budi kuungwa mkono ili yakamilike kwa wakati na sisi kama serikali tutahakikisha yanafanikiwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu husika.

Mapema wiki hii Mwanasheria wa Simba Evodius Mtawala, alifafanua namna ambavyo mfumo huo utafanya kazi kuanzia kwa mmiliki wa hisa nyingi Mo Dewji atakayemiliki asilimia 49 ya hisa huku wanachama wakimiliki 51%.

Kwa upande wa wanachama watamiliki hisa ndani ya kampuni ya 'Simba Sports Club Company Limited' kupitia kwa kampuni ya wanachama itakayoitwa 'Simba Sports Club Holding Company Limited' chini ya baraza la wadhamini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: