Sunday, 27 May 2018

Simba SC yawakosa nyota wake watatu


Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18, Simba SC kimeondoka Jijini Dar es Salaam kuelekea mjini Songea kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Majimaji FC kesho huku ikiwakosa nyota wake watatu.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizowekwa wazi na uongozi wa wekundu wa msimbazi ambapo imewataja wachezaji huo kuwa ni John Bocco, Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi na kusema lengo la kuwaacha nyota hao ni kutaka kuipumzisha miili yao ili waweze kupambana vilivyo katika michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza mwezi Juni 2018 nchini Kenya.

Kuelekea mechi hiyo dhidi ya Majimaji FC inayotarajiwa kuchezwa kesho Mei 28, 2018, uongozi Simba umesema hawaendi kuihurumia Majimaji bali wanaenda kuweka heshima ya kupigania matokeo yao kama walivyokuwa wanafanya hapo awali.

Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kufikia tamati kesho Mei 28, 2018 kwa kuchezwa michezo nane katika maeneo tofauti tofauti.

No comments:

Post a comment