Friday, 11 May 2018

Profesa Mwandosya: "Hongera Sugu umehitimu chuo cha uanasiasa gerezani"


Waziri wa serikali ya awamu ya nne Prof. Mark Mwandosya ameingia katika Orodha  ya watu walioonesha furaha yao baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kuachiliwa jana  kutoka gerezani ambapo alihukumiwa kifungo cha miezi mitano.

Prof. Mwandosya ameandika katika ukurasa wake wa twitter; “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa, gereza la Ruanda, Mbeya. Kutofautiana vyama, itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui. Mungu Ibariki Tanzania.”

No comments:

Post a comment