Mkazi wa Mbezi, Frank Japhet (23) amedaiwa kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, mkoani Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 20 aliodaiwa kuuiba kung’ang’ania kichwani.
Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo.
Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipotaka kuacha kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ndipo mzigo huo ulipomng’ang’ania kichwani.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Amesema, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini alishindwa na kunyanyuka nao kichwani.
Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.
Mpaka sasa yuko Kituo cha Polisi Mlandizi na mzigo wake kichwani akisubiri mwenye mali aliyoiiba ambaye tayari Jeshi la Polisi Mlandizi limemuita afike kituoni hapo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: