Thursday, 24 May 2018

Msukuma; Simu yangu ina historia kubwa nitaiweka Makumbusho

Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu amefunguka kuwa simu yake ina historia kubwa na endapo ikiharibika ataiweka katika kumbukumbu zake.

Musukuma amesema hayo kupitia KIKAANGONI ya East Africa Televisheni kuwa simu hiyo ilisababisha kuingia katika mgogoro na aliyekuwa mteja wake ambaye aliinunua dukani kwake na kushindwa kuitumia hatimaye kumpeleka Polisi.

“Simu yangu naipenda sana maana ina historia kubwa sana na ikitokea imeharibika nitaiweka kuwa ukumbusho katika chumba change cha kumbukumbu kwani ili sababisha kupelekwa Polisi na aliyekuwa mteja wangu wakati nafanya biashara ya kuuza simu”, amesema Musukuma.

Mh. Musukuma amesema kuwa hahitaji kuwa na simu nyingine zaidi ya hiyo na haoni mapungufu yoyote kwani inampatia kila kitu katika suala zima la mawasiliano.

No comments:

Post a comment