Vijana zaidi ya 200 wamepata ajira ya
kufanya utafiti wa athari za kijamii na kiuchumi katika njia ya Bomba
la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima Nchini Uganda hadi
katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Vijana
hao tayari wamepata mafunzo ya kazi yaliyotolewa jijini Dar es Salaam
na kampuni ya Digby Wells Consortium (DWC) kwa kushirikiana kampuni
nyingine za kitanzania na za kimataifa kama Digby Wells Environmental
( kampuni ya kimataifa yenye makao makao makuu nchini Afrika ya Kusini
na Uingereza) na Paulsam Geo-Engineering Ltd (Kampuni ya Kitanzania
inayotoa huduma za ushirikishwaji wadau, upimaji wa ardhi na watakwimu
wa mambo ya kijamii na uchumi ).
Kampuni
nyingine zilizotoa mafunzo kwa vjana hao ni Whiteknights Real Estate
Investment Analysts Ltd (kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za
uthamini) na STCL (kampumi ya Kitanzania inayotoa huduma za Afya na
usalama na usafiri kwa makampuni ya DWC).
Lengo
la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa wahusika uelewa wa kufanya
tathmini ya athari mbalimbambali za kiuchumi na kimazingira katika
maeneo yatakayopitiwa na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.
Mara
baada ya kumalizika kwa mafunzo husika, vijana wataanza kazi tarehe
16 Mei, 2018 chini ya kampuni ya kizalendo ya Paulsam ambayo ni
mkandarasi anayetekeleza kazi hiyo kwa kushirikiana na kampuni
nyingine.
Zoezi
hili litatekelezwa na Makundi 9 yatakayogawanyika katika Mikoa 8 bomba
linapopita, Wilaya 25, kata 132 na Vijiji Zaidi ya 280.
Aidha,
zoezi litahusisha kubaini athari za utwaaji ardhi kwa ajili ya Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), na kutengeneza
mifumo ya kuzuia, kupunguza na kudhibiti athari mbaya kwa watakaoguswa
na mradi, na kutengeneza mpango wa uhamishaji makazi kupisha Mradi wa
Ujenzi wa Boma la Mafuta
Kazi
hii inajumuisha ukusanyaji wa taarifa za ardhi na rasilimali kwa
ajili ya uthamini na hatimaye utwaaji wa ardhi ambayo itahitajika kwa
ajili ya ujenzi wa njia ya bomba la mafuta kabla ya muda wa kuanza
ujenzi.
Zoezi hili litahusisha pia, uorodheshaji wa mali zote zisizohamishika na makaburi ndani ya eneo lililochaguliwa na mradi.
Zoezi
litatekelezwa kwa kutumia teknolojia ya vifaa vya kisasa (tablets)
kuchukua na kutunza takwimu. Mwisho fomu yenye rekodi itatolewa na
kusainiwa na wahusika wote na nakala atapewa mhusika na kusaidia kubaini
namna wahusika watakavyokuwa wameathirika.
Katika
zoezi hilo vijana watafanya kazi kwa kushirikiana na wataalam kutoka
Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na
Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Post A Comment: