Tuesday, 29 May 2018


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akimshukuru meneja wa NMB kanda ya Ziwa,  Abraham Augustino  baada ya kupokea madawati ya shule ya msingi Mwenge kutoka NMB .
Katibu Tawala Wilaya ya Songwe, Johari Samizi (wa tatu kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa NMB kanda ya nyanda za juu, Focus Lubende baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni tano. 
Mkuu wa Wilaya ya Kahama (Mwenye kofia) Fadhili Nkurlu, akimshukuru meneja wa NMB kanda ya kaskazini,  Leon Ngowi  baada ya kupokea msaada wa  vifaa vya ujenzi. 

Sehemu ya  akina mama wakiwa na Meneja wa huduma za Jamii kutoka benki ya NMB, Lilian Kisamba wakiwa na furaha baada ya kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya hospitali hususani vitanda vya kujifungulia katika kituo cha Afya cha Mgango- wilayani Musoma.

Benki ya NMB Tanzania kupitia Kitengo cha Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) imetoa msaada wa vifaa vya hospitali, vifaa vya ujenzi wa madarasa pamoja na madawati katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Songwe na Mara.

Katika Mkoa wa Mwanza, Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 60 kwa Shule ya Msingi Mwenge wenye thamani ya Tsh. milioni tano ili kusaidia kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo.

Katika Mkoa wa Shinyanga, imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi ambavyo vitatumika kumalizia ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Nyasubi iliyopo wilayani Kahama.

Pia NMB imetoa msaada kwa Mkoa wa Songwe kwa kutoa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Tsh. milioni tano ambavyo vitatumika katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe Mwambani, vifaa hivyo vinalenga kupunguza uhaba wa vifaa uliopo katika hospitali hiyo.


Hata hivyo NMB haikuishia hapo kwani pia imetoa vifaa vya hospitali vikiwepo vitanda vya kujifungulia katika kituo cha Afya cha Mgango kilichopo wilayani Musoma, Mara.

Kwa mujibu wa Meneja wa Miradi na Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Bi. Lilian Kisamba alisema benki hiyo imetenga Tsh. bilioni moja kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.

No comments:

Post a comment