Tuesday, 29 May 2018

Mbunge Kingu Atoa ujumbe mzito wa kumuaga Kinana

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mkoani Singida Mh: Elibariki Kingu amemuaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu jana  kuwa wataendelea kumuenzi kwa kuwasaidia kuwa viongozi bora. 

Kingu ametoa ahadi hiyo kwa Kinana ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambayeni  Rais wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Pamoja na hayo Mbunge Kingu ameweka wazi kumtambua kinana kama shujaa aliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma. 


"Uongozi wa upendo na unyenyekevu na kuwasaidia watu kuimarika kuwa viongozi bora ndio kunatufanya wana CCM kusema kinana alikua shujaaa na atabaki kuwa shujaa katika chama chetu"

 Habarika sasa kwa kupitia Msumba News Blog kwa kupakua App yetu kwa kubonyeza hapo chini. 
==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

No comments:

Post a comment