Monday, 21 May 2018

Man U yaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Chelsea


Klabu ya Manchester United imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Chelsea, Willian msimu huu ili kuhakikisha inaimarisha kikosi chake kwaajili ya michuano mbalimbali.

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa kiungo huyo wa timu ya taifa ya Brazili anahitaji kuondoka msimu huu endapo meneja wa timu hiyo, Antonio Conte atasalia Stamford Bridge.

Mpaka sasa Willian amesaliwa na miaka miwili kwenye mkataba wake na Blues na hivyo kuhusishwa kutimkia United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye amepigiwa kura na wachezaji wenzake kuwa mchezaji bora wa msimu ndani ya klabu hiyo ameanza kukosekana kwenye kikosi cha kwanza kilichoanza dhidi ya United mchezo wa fainali wa FA huku ikiwa ni kwamara yake ya nne kuanzia benchi kwenye mechi tano zilizopita.

Willian amefunga jumla ya mabao 44 katika michezo 236 aliyocheza Chelsea tangu kujiunga kwake akitokea Urusi kwenye klabu ya Anzhi mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment