Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa siku 14 kwa upande wa mashtaka
kuhakikisha wanakamilisha kuchapa maelezo ya washtakiwa wa kesi ya
kumiliki mali zisizoendana na kipato, inayomkabili mhasibu mkuu wa
Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na
wenzake watatu.
Baada
ya kupitia maelezo ya pande zote, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo
hadi Mei 30, 2018 na kuutaka upande wa mashtaka kuhakikisha
wanakamilisha kuchapa maelezo hayo ili washtakiwa hao waweze kusomewa
maelezo ya awali
Mbali
na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga,
Leonard Aloys na Yasini Katera na wote wanakabiliwa na mashitaka 43
yakiwemo 20 ya utakatishaji wa fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana
na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo
mbalimbali.
Uamuzi
huo umetolewa leo Mei 16, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo,
Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara saba,ikiwa
katika hatua ya kuwasomea hoja za awali (PH), washtakiwa hao.
Hatua
hiyo, inatokana na upande wa mashtaka kuieleza Mahakama hiyo kuwa wapo
katika hatua za mwisho za kuchapa maelezo ya washtakiwa.
Awali,
wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amedai mahakamani hapo kuwa kesi
hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini
walikuwa hawajakamilisha uchapaji wa maelezo ya washtakiwa hao.
“Kesi
imekuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kuwasomea maelezo ya awali
washtakiwa wote , lakini tunaiomba Mahakama itupe ahirisho la mwisho ili
tuweze kukamilisha uchapaji wa maelezo ya washtakiwa,” amedai wakili
Peter.
“Tayari
maelezo ya washtakiwa tumeshaanda na kilichobaki ni kuchapwa tu, hivyo
tunaiomba Mahakama yako itupe ahirisho la mwisho.”
Baada
ya maelezo hayo, wakili wa utetezi, Semi Malimi na Alex Mgongolwa
wamedai kuwa maelezo ya awali yameahirishwa kusomwa kwa zaidi ya mara
saba kuanzia April 4, 2018.
Post A Comment: